Posts

Showing posts from November, 2017

BAWASIRI NI NINI?

Image
Bawasiri ni ugonjwa ambao unatokana na kuathirika kwa mishipa ya sehemu ya ndani na nje ya tundu la haja kubwa na wakati mwingine kutoa damu wakati wa kutoa haja kubwa. Ugonjwa huu unasababisha muwasho na maumivu makali katika tundu la haja kubwa.  Mara nyingi tatizo hili huwapata watu kuanzia umri wa miaka 30 – 70.    Kuna aina mbili za bawasili : Bawasiri ya Ndani : Hiki nikinyama kinachootea ndani kabla hakijatokea njee. Bawasiri ya Nje : Hiki nikinyama au kivimbe kinatokea nje baada yakutokea ndani. Kinatokea njee kwawalio athirika, na ukikaa muda mrefu na huu ugonjwa unajiongozea matatizo ya kiafya ambayo siyo rahisi kukabiliana nayo, na maranyingi ugonjwa huu unasababisha vifo vya ghafla.                                   II.          CHA...

FAHAMU AFYA YA TEZI DUME (PROSTATE GLAND)

Image
Kila mwanaume anazaliwa na Tezi dume. Tezi dume siyo ugonjwa bali ni kiungo kama viungo vingine mwilini. Tezi dume inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa nikutengeneza majimaji ya uzazi wa mwanaume (shahawa), ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizo tengenezwa kutoka kwenye Korodani; na husaidia mbegu za kiume kubaki hai kwa muda unaostahili. Tatizo linakuja kiungo hiki kinapoanza kutanuka. Kiungo hiki kinatanuka taratibu taratibu mnoo. Hili ni tatizo linalo wakumba wanaume wengi. Takwimu zinaonesha kwamba kati  ya wanaume 10, wa 5 na kuendelea wana dalili za kutanuka kwa Tezi dume. Ukuwaji wa Tezi dume ni ile hali ya chembe chembe hai katika tezi ya kiume kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili katika eneo linalo zunguka mirija ya kupitisha mkojo na mbegu za kiume. Tatizo hili kwa sasa linawapata wanaume kuanzia umri wa miaka 25 na kuendelea, tofauti na awali lilikuwa miaka zaidi ya 50. Takwimu...